Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 8:54 am

NEWS: CHINA YADAI KUMSHIKILIA MKUU WA INTERPOL

Taarifa kutoka nchini China Jana zinasema kuwa mamlaka za serekali hiyo zimethibitisha kuwa zinamzuia mkuu wa Interpol Meng Hongwei aliyepotea tangu mwanzoni mwa juma hili kwa madai kuwa alikuwa anachunguzwa na tume ya kupambana na rushwa nchini humo kwa ukiukaji wa sheria.

Meng, ambaye pia ni naibu waziri wa wizara ya usalama wa umma China, aliarifiwa kupoeta baada ya kusafiri kutoka mji wa Lyon Ufaransa , kuliko na makao makuu ya Interpol kwenda China mnamo Septemba 25.

Interpol imesema imepokea barua ya kujiuzulu kwake mara moja kutoka kwa ofisi ya rais.

Familia yake Meng haijawasiliana naye tangu andoke katika makao hayo makuu ya Interpol nchini Ufaransa

Gazeti la South China Morning Post lilinuku taarifa zilizosema kuwa Bw Meng, 64, alipelekwa kwenda kuhojiwa nchini China.

Haijulikani ni kwani nini alikuwa anachunguzwa na mamlaka za nidhamu au alikuwa anazuiliwa wapi.