Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 5:54 am

NEWS: CHAMA CHA MUGABE CHASHINDA URAIS ZIMBABWE

Harare: Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Zimbabwe (ZEC) usiku wa kuamkia leo imetangaza matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Zimbabwe, baada ya uchaguzi mkuu kufanikiwa kufanyika salama Julai 30, 2018.

Emmerson Mnangagwa wa Zanu-PF ameshinda Urais wa Zimbabwe katika uchaguzi wa kwanza wa Urais, baada ya Robert Mugabe kuondoka madarakani, Mnangagwa ameshinda kwa kupata zaidi ya aslimia 50 ya kura zote dhidi ya mpinzani wake Nelson Chamisa kutoka MDC.

ZEC wametangaza kuwa Emmerson anashinda kiti hicho kwa kupata ushindi wa asilimia 50.8 ya kura zote halali zilizopigwa wakati mpinzani wake wa karibu kutoka MDC Nelson Chamisa akipata asilimia 44.3 ya kura zote.

Kumekuwa na sintofahamu nchini Zimbabwe baada ya Tume ya uchaguzi nchini humo kuchelewesha kutangaza matokeo hali iliyopelekea kusababisha maandamano kutoka kwa wafuasi wa Chamasi.

Waangalizi wa uchaguzi pia walilazimika kushinikiza ZEC kutangazwa kwa matokeo hayo.