- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: CHADEMA YATAKA KUMSAJILI MAALIM SEIF KWENYE SAFU YA UWONGOZI
Chama cha Demokrasia na Maendelo Chadema kimeendelea kufanya mipango yake ya kutaka kumshawishi Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharrif Hamad Kujiunga na chama hicho hivi karibuni.
Chadema imetanabainisha kuwa Makamu huyo wa kwanza wa zamani wa Rais katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (2010-2015), inamtaka ili awe mgombea wao katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 visiwani Zanzibar.
Kauli hiyo imetolewa na Baraza la wazee Chadema Visiwani Zanziba kupitia Mwenyekiti wa Baraza hilo, Hashimu Issa Juma, limekuja katika kipindi ambacho chama cha CUF kimekumbwa na mgogoro wa uongozi tangu mwaka 2015.
Mgogoro wa CUF umekuja baada ya Mwenyekiti anayetambulika na ofisi ya msajili Profesa Ibrahim Lipumba kujiuzulu wadhifa wake kuelekea uchaguzi mkuu kisha mwaka 2017 kurejea kwenye cheo hicho kiujanja ujanja licha ya kueleza kuwa baadhi ya wanachama wamemuomba arudi madarakani.
Kurudi kwa Lipumba ndani ya Cuf kumetengeneza makundi mawili. Kundi la wanaomuunga mkono Profesa huyo na jingine likiwa upande wa Maalim Seif.
Mvutano unaosababishwa na makundi hayo unaonekana kuwa mkubwa. Kuna dalili kkwamba huenda ulichangia baadhi ya viongozi akiwemo Julius Mtatiro akikihama chama hicho pamoja na wabunge wa viti maalumu waliomuunga mkono Maalim Seif kupoteza ubunge wao.
Nia ya baraza la wazee wa Chadema imetafsiriwa kuwa mbinu ya kuongeza ushawishi wao katika siasa za Visiwani Zanzibar kwa kuwa chama hicho hakina nguvu za kutosha wala kuwa na mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa visiwani hum