Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 2:25 pm

NEWS: CHADEMA YASUSIA UCHAUZI WA MADIWANI TENA

Arusha: Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema kupitia kwa mwenyekiti wake Taifa Freeman Mbowe kimetangaza kususia uchaguzi wa kata 5 zilizopo katika wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha kwa madai ya ukiukwaji wa sheria, kanuni na Taratibu za uchaguzi.

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe

Akiongea na waandishi wa habari jana Juma pili (26.11.2017) Mwenyekiti wa chadema Bw. Freeman Mbowe amewataka madiwani, viongozi wa chama na mawakala wote wa chama wasishiriki kwa namna yoyote katika uchaguzi wa kata 5 za Arumeru " Tunawaagiza madiwani wetu wote na viongozi wetu wa chama immediately wajitoe katika uchaguzi wa Arumeru, mawakala wetu wote ambao wamekuja kuigia vituoni mchana huu baada ya kura zimeshakuwa fault waondoke wote vituoni"

wananchi wa Arumeru wakipiga kura

Mbowe alisema kuwa baada ya kutokea kwa sintofamu hiyo amejaribu kuwasialiana na mkurugezi wa Uchaguzi ili aweze kupata mwongozo "nimewasiliana na mkurugezi mkuu wa tume ya uchaguzi, Bw. kailima amenambia yupo tunduru, nimemueleza mapungufu haya yote, namengine mengi ambayo yapo katika kata zingine mbalimbali za nchi. lakini kama nilivyosema awali, viwango vinatofautiana. tutaendelea kushiriki katika chaguzi hizo kata zingine 38 zilizobaki" alisema mbowe

Mkurugezi mkuu wa tume ya Uchaguzi Bw. kailima Ramadhani

Mbowe amesema kuwa kinacho fanyika Arumeru sio uchaguzi tena ni vurugu watu wanatekwa hovyo akitolea mfano wa mbunge wa Babati mjini Paulina Gekuli amekamatwa na hadi sasa hajulikani alipo, sasa kutoka na hali hiyo mbowe ameitaka tume ya uchaguzi kuitisha uchaguzi upya.

Jeshi la polisi likiweka Doria