Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 12:46 pm

NEWS: CHADEMA YAIBUA MAPYA KWENYE CHAMA CHAO.

DAR: Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimezindua kitabu cha sera za chama hicho toleo la mwaka 2018 ikiwa na sera 12 ambazo zimezungumzia namna ambavyo chama hicho kimejipanga kuinua maisha ya mtanzania na taifa kwa ujumla.

Akizungumza leo Septemba 25, 2018 wakati wa uzinduzi huo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema sera hizo zitakuwa zinafanyiwa marekebisho kulingana na wakati.


Amesema eneo la kwanza lililoko kwenye sera hiyo ni ile inayolinda uhuru wa wananchi.


Mbowe amesema Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kuzungumzia suala la maendeleo ya watu na uhuru, jambo ambalo wamelijadili kwa kina kwenye sera hiyo.


“Mwalimu Nyerere alisema sera za Chadema zilikua sera za kuinua maisha ya watanzania, kwa hiyo chama chetu sio chama cha kutafuta uhuru, bali sera zetu zimejikita zaidi kuhakikisha kila mtanzania anakua na maisha bora, sera hizi zimelenga maeneo 12 na tutaweza kuzifanyia marekebisho mara kwa mara pindi zitakapohitajika pia ni ruhusa kunakiliwa na vyama vingine.”


Amelitaja eneo lingine ni nafasi kuwa na sera zinazolenga misingi ya uchumi.


Amesema katika eneo hilo wameainisha ni kwa namna gani wananchi watapata huduma za kijamii.


Amefafanua eneo hilo limeainisha namna uchumi utakavyokuwa endelevu badala ya kuwa uliohodhiwa na Serikali.


Mbowe ameitaja sera nyingine ni zinazoilinda na kuihuisha jamii kupata huduma ya maji, barabara yasiwe mambo yanayofanywa na sekta binafsi bali yafanywe na Serikali.


"Sasa hivi kumejengeka dhana kuwa Serikali uliyojenga shule, zahanati inakuwa ni kama msaada, hii si sawa hayo ni majukumu ya Serikali," amesema Mbowe.


Mbowe amesema kabla ya kutayarisha sera hiyo wametumia mwaka mzima kufanya tafiti na kukusanya maoni kutoka kwa watu mbalimbali.