- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : CHADEMA WATAKA SERIKALI IKOSOLEWE INAPOKOSEA KATIKA SHUGHULI ZAKE
CHADEMA yawataka viongozi wa dini kuendelea kuikosoa serikali ya Tanzania
Chama Kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Demokrasia ya Maendeleo (CHADEMA) kimewataka viongozi wa dini kupuuza vitisho dhidi yao na badala yake waendelee kuikosoa serikali ya Rais John Pombe Magufuli.
Wito huo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) umetolewa na Mwenyekiti Taifa wa chama hicho Freeman Mbowe alipoongea na waandishi wa habari jijini Dare Salaam na kuwawataka viongozi wa dini kuendelea kuikosoa serikali na wasitishwe na mtu yoyote kwani bila wao kusema jamii ya Watanzania itaangamia.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ametoa kauli hiyo wakati alipozungumzia mambo mbalimbali yanayotokea nchini Tanzania na hali ngumu ya maisha ya Watanzania ilivyokuwa mwaka 2017 uliomalizika jana ambapo aliwanyooshea kidole cha lawama watendaji wa serikali ya Rais John Magufuli.
Mwenyekiti wa Chadema aidha amekosoa vikali hatua ya serikali ya Tanzania ya kuwatisha viongozi wa dini na kuwataka wasiikosoe serikali ya nchi hiyo na kubainisha kwamba, viongozi wa dini wanapaswa kuikosoa serikali na kutoa miongozo inayofaa kwa ajili ya kuboresha utendaji wa serikali.
Aidha Freeman Mbowe amesema: Viongozi wa dini msiingize roho ya uoga, mtaiponya nchi, mkikaa kimya nchi itakufa, nchi inateketea, nchi inaangamia viongozi wa dini msikae kimya watu wanauawa.
Kauli hiyo ya Mbowe imekuja siku chache baada ya serikali kutishia kuwashughulia viongozi wa dini wanaojihusha na masuala ya siasa na kuikosoa serikali ambapo wametakiwa kutojihusha na masuala ya siasa.