Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 1:34 am

NEWS: CCM YAWATIMUA MAKATIBU WENEZI KWA KULAWITI NA KUMPA UJAUZITO MWANAFUNZI

Mwanza: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Nyamagana kimewavua uongozi Makatibu wa Siasa na Uenezi wa kata za Buhongwa na Mkolani wilayani humo kwa tuhuma na makosa ya kukidhalilisha na kukichafua kwenye jamii.Salum kalli mwenyekiti Wilaya Nyamagana

Inadaiwa kuwa Katibu wa Siasa na Uenezi wa Kata ya Buhongwa Hassani Bushagama, anadaiwa kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha tatu wa shule moja ambayo haikutajwa ambapo alitoroka na kutokomea tangu Julai mwaka huu.

Pia chama kimelaani matukio hayo yaliyofanywa na viongozi hao wasio na hofu ya Mungu,katiba na sheria za nchi ambao wanakiangusha CCM kwa kufanya vitendo viovu na mambo ya ovyo yanayodhalilisha.

Akitoa tamko la kuwavua nyadhifa za uongozi makatibu hao wa Uenezi kwenye mkutano wa dharura wa Kamati ya Siasa ya Wilaya mbele ya vyombo vya habari Jana November 1 Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana Salum Kalli alisema viongozi wa namna hiyo hawatavulimiwa kwa sababu wanafedhehesha chama.

“CCM inalaani vikali mambo yaliyofanywa na viongozi hao kwenye jamii na hatua hii itakuwa fundisho kwa viongozi wenye tabia kama hizo,maana si utamaduni na maadili ya CCM kwani inawataka wawe waadilifu na waaminifu kwenye nafasi zao.Hivyo tutafuatilia tabia, mienendo na maadili ya kila kiongozi wa CCM aliyepo madarakani,”alisema.

Kalli alieleza kuwa Kamati ya Siasa ya Wilaya imechukua hatua hiyo na kutoa tamko hilo Watanzania wajue ili viongozi wenye tabia chafu zisizofaa kwenye jamii waache kwa kuwa CCM haitawavumilia.