- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: CCM YATOA RAMBIRAMBI YA MILIONI 10 MV NYERERE
Dar es Salaam: Chama cha Mapinduzi (CCM) kimechangia Tsh. Milioni 10 kwa wahanga wa ajali ya Kivuko cha MV Nyerere kilichotokea mnamo Septemba 20 mwaka huu katika kijiji cha Ukara wilayani Ukerewe katika mkoa wa Mwanza.
Mchango huo umewakilishwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole kwa niaba ya chama hicho huku akisema kuwa wao kama chama wameguswa na msiba huo na kitaendelea kutoa mchango kadri watakavyopata.
"Tunawashukuru wote wanaoendelea kujitolea katika kuchangia waathirika hawa na Mungu aendelee kuwabariki," amesema Polepole.
Kwa upende wa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema mpaka sasa Sh300 milioni zimechangwa na Watanzania na taasisi mbalimbali kupitia akaunti iliyotangazwa.
"Hiyo itakuwa ni siku maalumu kwa ajili ya kuwaombea wapendwa wetu kwa imani ya dini zote kama ilivyokuwa katika ajali nyingine zilizowahi kutokea," amesema Majaliwa.