- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: CCM YASHINDA JIMBO LA BUYUNGU
Kigoma: Aliyekuwa waziri wa Kilimo na Ufugaji Christopher Chiza amefanikiwa kushinda uchaguzi mdogo wa Marudio uliofanyika jana Jumapili Agosti 12, 2018, baada ya kuwashinda wagombea wengine akiwemo Mgombea wa Upinzani wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Eliya Michael
Chiza (CCM) amepata kura 24,578 akifuatiwa na Eliya (CHADEMA) aliyepata kura 16,910.
Akitangaza matokeo hayo leo Jumatatu Agosti 13 saa 11 alfajiri, msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo, Lusubilo Mwakabibi amemtangaza Chiza kuwa mshindi. Vyama vingine na kura walizopata ni Demokrasia Makini (11), UMD (12), NRA (17), UPDP (18), DP (22), AFP (51) na ACT – Wazalendo kura 100. Mwakabibi amesema idadi ya waliojiandikisha kupigakura ni 61,980, waliopiga kura ni 42,356, kwamba kura halali zilikuwa 41,841 na zilizoharibika 515.
Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Chiza amesema yupo tayari kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo na kuwaahidi utumishi uliotukuka. Amesema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazohitaji ufumbuzi na akiapishwa ataanza nazo mara moja. Awali, Eliya amesema mawakala wake hawakuitwa kwenda kujumlisha matokeo hayo, kubainisha kuwa uchaguzi huo ulikuwa na mazingira magumu.
Amesema matokeo aliyonayo kutoka katika kila kituo, hayafanani na yaliyotangazwa. “Kwa umri nilionao najiona mshindi wa uchaguzi huu, nimejifunza mengi na umenijenga kwa kiwango kikubwa. Nimeshinda kwa kura za watu ili wao wameamua kumtangaza mtu wanayemtaka,” amesema