- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: CCM YABEBA VITI VITATU VYA UDIWANI UCHAGUZI WA MARUDIO
Kilimanjaro na Mbeya: Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaonekana kupata ushindi mkubwa katika udiwani na hata Ubunge baada ya chama hicho mpaka sasa kushinda kata tatu.
Kwa mujibu wa Msimamizi wa Uchaguzi katika jiji la Mbeya Mjini, James Kasusura amemtangaza Newton Mwatujobe wa CCM kuwa diwani mteule wa Maanga kuwa mshindi dhidi ya Steven Mwashilindi wa Chadema.
Waliojiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura ni 6,292, waliojitokeza kupiga kura ni 3,600.
Kasusura amesema kuwa Mwatujobe amepata kura 1,897 huku mpinzani wake Mwashilindi akipata kura 1,703. Kasusura amemkabidhi cheti cha ushindi diwani huyo mteule.
Uchaguzi kaskazini
Msimamizi wa Uchaguzi, kata ya Machame Uroki, Msafiri Msuya amemtangaza Robson Kimaro wa CCM kuwa diwani mteule wa kata hiyo kwa kupata kura 2,174
Katika uchaguzi huo Kimaro, alikuwa akichuana na Elibashiri Kombe wa Chadema ambaye amepata kura 704.
Amesema waliojiandikisha kupiga kura 4,512, waliopiga kura ni 2896, kura halali 2,878 huku zilizoharibika zikiwa 18.
Msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Kia, Saimon Egid, amemtangaza Yohana Laizer wa CCM kuwa diwani mteule wa Kata ya Kia kwa kupata kura 1,367 huku mgombea wa Chadema, Hassan Ibua akipata kura 230