- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BURUNDI YAKATAA KUSHIRIKI MAZUNGUMZO YA AMANI DHIDI YA UPINZANI
Bujumbura: Serikali ya Burundi inasema haitaweza kushiriki katika mazungumzo ya amani kuhusu nchi hiyo yanayofanyika mjini Arusha nchini Tanzania kwa kuwa nchi hiyo iko katika maombolezo ya mwezi mzima kuwakumbuka mashujaa wa taifa hilo kwa mujibu wa Evariste Ndayishimiye Katibu Mkuu wa chama tawala cha CNDD-FD
Burundi inatoa kauli hiyo Wakati mazungumzo ya amani kuhusu Burundi yakitarajiwa kuanza siku ya Jumatano mjini Arusha nchini Tanzania, tayari yameingia dosari baada ya Serikali ya Bujumbura, pamoja na vyama washirika, kutangaza kuwa hawatashiriki.
Kwa upande wao muungano wa upinzani wa ndani ya Burundi “AMIZERO YA BARUNDI” unaoongozwa na Agathon Rwassa, umeeleza kushangazwa na hatua ya Serikali, ukisema utawala unatafuta sababu ili kukwepa mazungumzo ya Arusha.
Uamuzi huu wa Serikali umekashifiwa vikali na muungano wa wapinzani wanaoishi nje ya Burundi “CENARED” ambao unasema kuwa haijawahi kutokea maombolezo haya yanayosemwa na Serikali kufanyika kwa mwezi mzima na kwamba hizi ni njama za Serikali kutoshiriki.
Jean Minani Mwenyekiti wa muungano wa CENARED na anasisitiza kuwa njia pekee ya kupata suluhu ni kupitia mazungumzo ya kweli.
Mazungumzo ya haya yanatajwa kuwa huenda yalikuwa ni ya mwisho katika kuelekea kupata muafaka kuhusu maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Kutoshiriki kwa Serikali ya Burundi, kunaelezwa kuwa ni pigo kubwa kwa mratibu wa mazungumzo rais wa zamani wa Tanzania, Benjamin Mkapa.