- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BUNGE LAPITISHA TAARIFA YA UCHAMBUZI WA SHERIA NDOGO .
BUNGENI DOM: Bunge limepitisha taarifa kuhusu uchambuzi wa sheria ndogo huku likiazimia kuwa wizara zote ambazo sheria zake ndogo zimebainika kukinzana na masharti ya sheria mama au sheria nyingine kufanyia marekebisho sheria hizo ili kuondoa vifungu vinavyokwenda kinyume na masharti yaliyopo.
Azimio hilo limewasilishwa leo bungeni jijini Dodoma na mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya sheria ndogo Andrew Chenge wakati akiwasilisha taarifa kuhusu uchambuzi wa sheria ndogo zilizowasilishwa katika mkutano wa kumi na mkutano wa kumi na moja wa bunge.
Chenge amesema kukinzana huko kunaifanya kanuni husika kuwa batili kwa kiwango ilichokinzana.
Chenge ametaja moja ya sheria ndogo iliyobainika kuwa na dosari na kwenda kinyume na sheria mama na sheria nyingine za nchi kuwa ni sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi sura ya 328 inayompa waziri wa fedha jukumu la kushiriki katika majadiliano ya mikataba ya kugawana mapato katika sekta ndogo ya mafuta na gesi asilia nchini.
Wakichangia taarifa hiyo baadhi ya wabunge wametoa ushauri wa kushirikisha wadau mbalimbali katika utunzi wa sheria ndogo ili kusiwe na changamoto wakati wa utekelezaji kama wanavyochangia mbunge wa viti maalum Zainab Katimba na mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete.