Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 3:43 pm

NEWS: BUNDUKI YA MBUNGE NASSARI YACHUNGUZWA NA POLISI

Dar es salaam: Kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema wameanza uchunguzi wa kina katika tukioa la uvamizi kwenye nyumba ya mbunge Joshua Nassari ili kubaini endapo kulikuwa na tukio au la na tunaichunguza na bunduki yake kwanza.
“Tunaifanyia uchunguzi bunduki yake, tunataka kujiridhisha endapo kulikuwa na tukio au la,” alisema Mkumbo.
Mkumbo alisema msako unaendelea ili kuwabaini washukiwa na kwamba hawajapata maganda ya risasi zinazodaiwa kutumika katika uvamizi huo.

Siku ya Jumamosi Tarehe (02.11.2017) Nassari aliwaambia waandishi wa habari kuwa alisikia hali isiyo ya kawaida ndani ya uzio wa nyumba na baadaye kulisikika milio ya risasi. Alisema mbwa wake aliyekuwa akibweka alinyamaza, hali iliyomfanya achukue silaha yake kujihami.
“Nilipiga risasi tano, kisha kukawa kimya nikaenda kuwaamsha vijana wanaonisaidia hapa nyumbani kuwaeleza tukio lililotokea kisha nikaondoka.”

Alisema waliofanya tukio hilo hawakujua kama ana silaha kwa sababu mwaka 2014 wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa, bastola yake ilichukuliwa na polisi na hadi leo haijarudishwa, hivyo kuwa na silaha nyingine kulimsaidia kujibu mapigo.

Katika tukio hilo, Nassari alisema aliwajibu watu hao kwa kupiga risasi tano hewani huku wenyewe wakipiga 12 na moja ilimpata mbwa wake ambaye alimzika juzi katika maeneo ya nyumba anayoishi.