- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BOMOA BOMOA YAWALIZA WAMACHINGA NJOMBE
Njombe: Jana wananchi wa Chaugingi katika halmashauri ya Mji na Mkoa wa Njombe, wameishutumu serikali kupitia dalali ambaye anaondoa vibanda vya wafanyabiashara wadogo pembezoni mwa barabara za mji huo kwa kutotoa elimu kwa wafanyabiashara juu ya uvunjaji wa vibanda na meza za biashara
Wakizingunza kwa nyakati tofauti jana, watu hao walisema ubomoaji huo umekuwa wa ghafla kwa kuwa awali walikuwa wakipatiwa taarifa lakini haikufanyika hivyo.
“Mimi niliambiwa tu niondoe meza, nimeondoa lakini banda langu hawakuniambia nilivunje kwa hiyo leo asubuhi (jana) nikashangaa wanakuja kuvunja hapa wameanza kwa wengine ambao hawakuwa wamevunja meza zao lakini nashangaa wamevunja mpaka kibanda changu,” alisema Margaret Mayemba
Kazi ya kuondoa wafanyabiashara pembezoni mwa barabara lililoendeshwa kuanzia jana, limelenga kuwaondoa watu wasio na maduka bali wenye mabanda au meza za kuuza mboga, mafuta na matunda lengo likiwa ni kuwalazimisha kwenda katika soko la Joshoni ambalo sasa limekuwa razima kuhamia huko.
Wafanyabiashara wadogo walioathirika na bomoabomoa walisema wamekuwa wakilazimishwa kwenda huko bila kuwapo elimu na kuwa Watanzania wa sasa ni tofauti wa wale wa zamani kwa sababu ni wepesi wa kuelewa.
Kwa maana hiyo, walisema elimu ilikuwa kitu cha msingi na wangeambiwa mipaka wanayotakiwa kuishia, wasingepata shida ya kuanza kubomboa.
Jordan Mayemba, mmoja wa wakazi walioshuhudia bomoabomoa hiyo, alisema kisosi hicho cha bomoabomoa kimetumia nguvu kubwa kiliko ambavyo kingejikita kutoa elimu na kwamba wamesababisha uharibifu wa mali, vikiwamo vitanda na mabati.
“Ukishatoa elimu watu wanaelewa kwani si wabishi. Wangetanguliza elimu lakini kuwatoa kwa nguvu si ustaarabu na walitoa taarifa lakini hawakusema inatakiwa kuishia wapi,” alisema.
Mmoja wa waathirika wa bomoabomoa hiyo, na mkazi wa mtaa wa Idundilanga, Emmanuel Sanga, alisema katika mtaa huo pia wanawalalamikia viongozi ambao wanadaiwa kutotoa elimu kwa wakazi, hivyo kuwasababishia hasara ya mali zao.