- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BOMBA LA MAFUTA AFRIKA MASHARIKI LATOA AJIRA 200 ZA AWALI
Dar es salaam: Zaidi ya Vijana 200 wamefanikiwa kupata ajira za kwanza kabisa za kufanya utafiti wa athari za kijamii na kiuchumi katika njia ya Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima Nchini Uganda hadi katika Bandari ya Tanga nchini Tanzania.
Jana Mei 15 Vijana wote hao waliopata ajira hizo wamepatiwa mafunzo ya kazi yaliyotolewa jijini Dar es Salaam na kampuni ya Digby Wells Consortium (DWC) kwa kushirikiana kampuni nyingine za kitanzania na za kimataifa kama Digby Wells Environmental ( kampuni ya kimataifa yenye makao makao makuu nchini Afrika ya Kusini na Uingereza) na Paulsam Geo-Engineering Ltd (Kampuni ya Kitanzania inayotoa huduma za ushirikishwaji wadau, upimaji wa ardhi na watakwimu wa mambo ya kijamii na uchumi ).
Kampuni nyingine zilizotoa mafunzo kwa vjana hao ni Whiteknights Real Estate Investment Analysts Ltd (kampuni ya Kitanzania inayotoa huduma za uthamini) na STCL (kampumi ya Kitanzania inayotoa huduma za Afya na usalama na usafiri kwa makampuni ya DWC). Lengo la mafunzo hayo lilikuwa ni kuwapa wahusika uelewa wa kufanya tathmini ya athari mbalimbambali za kiuchumi na kimazingira katika maeneo yatakayopitiwa na Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki.
Mara baada ya kumalizika kwa mafunzo husika, vijana wataanza kazi tarehe 16 Mei, 2018 chini ya kampuni ya kizalendo ya Paulsam ambayo ni mkandarasi anayetekeleza kazi hiyo kwa kushirikiana na kampuni nyingine. Zoezi hili litatekelezwa na Makundi 9 yatakayogawanyika katika Mikoa 8 bomba linapopita, Wilaya 25, kata 132 na Vijiji Zaidi ya 280.
Pia utafiti huo utahusisha kubaini athari za utwaaji ardhi kwa ajili ya Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), na kutengeneza mifumo ya kuzuia, kupunguza na kudhibiti athari mbaya kwa watakaoguswa na mradi, na kutengeneza mpango wa uhamishaji makazi kupisha Mradi wa Ujenzi wa Boma la Mafuta Kazi hii inajumuisha ukusanyaji wa taarifa za ardhi na rasilimali kwa ajili ya uthamini na hatimaye utwaaji wa ardhi ambayo itahitajika kwa ajili ya ujenzi wa njia ya bomba la mafuta kabla ya muda wa kuanza ujenzi.
Zoezi hili litahusisha pia, uorodheshaji wa mali zote zisizohamishika na makaburi ndani ya eneo lililochaguliwa na mradi. Zoezi litatekelezwa kwa kutumia teknolojia ya vifaa vya kisasa (tablets) kuchukua na kutunza takwimu. Mwisho fomu yenye rekodi itatolewa na kusainiwa na wahusika wote na nakala atapewa mhusika na kusaidia kubaini namna wahusika watakavyokuwa wameathirika. Katika zoezi hilo vijana watafanya kazi kwa kushirikiana na wataalam kutoka Wizara ya Nishati, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC)