- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BINTI WA KIDATO CHA PILI AJINYONGA SIKUKUU YA MWAKA MPYA
Msichana wa kidato cha pili katika kijiji cha Nyaisero kwenye kaunti ya kisii Nchini Kenya amejiua Mwenyewe jana siku ya Mwaka mpya majira ya asubuhi.
kiongpozi wa eneo hilo Chief David Nyanchong'i amesema kuwa alijiuwa kwa kutumia kipande cha kitambaa ndani ya ya chumba chake wakati ndugu zake wakipata chai ya asubuhi baada ya kutoka kanisani katika kusherekea mwaka mpya.
Kwamujibu wa kiongozi huyo anasema familia yake ilikwenda kanisani asubuhi kwa minajili ya kusherekea sikukuu ya mwaka mpya na waliporudi nyumbani kwao msichana huyo akawaandalia chakula kama ilivyo kawaida yake, sasa mara baada ya kuwaandalia chai msichana huyo aliwaacha familia yake na kwenda chumbani kwake.
Alichelewa kurudi kwa muda kwenye meza ya chakula kuungana na familia yake, ndipo baadhi ya ndugu zake walipokwenda kumuangalia kutaka kujua anafanya nini kiasi cha kumfanya kuchelewa muda wote huo, ndipo wakaukuta mwili wake umeanguka sakafuni na alikuwa tayari ameshafariki dunia.
Mkuu wa polisi wa Ogembo alitembelea eneo la tukio na kuuondosha mwili wake mpaka kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Nyamache.
Polisi wanasema wanaendelea na uchunguzi kujua chanzo cha binti huyo kujiua.