Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 8:54 pm

NEWS: BENKI KUU YAKIRI KUPOROMOKA KWA SHILINGI YA TANZANIA

Dar es salaam: Thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani yadaiwa kuporomoka na kufikia kiwango cha chini zaidi katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita ukilinganisha na vipindi vingine huko nyuma.

Benki kuu imekiri mporomoko huo kupitia Mkurugenzi wa Masoko na Fedha BoT, Alexander Mwinamila ambaye aliliambia Gazeti la The Citizen la Tanzania kuwa kuporomoka huko kulitarajiwa.

"Hali ya sasa si kitu cha kustaajabisha na kwa kiasi imechangiwa na kuimarika kwa dola dhidi ya sarafu nyengine kwa siku za hivi karibuni." alisema Mwinamila

Aidha, sababu nyingine ni kushuka kwa mauzo ya bidhaa nje ya nchi na kuingia kwa fedha za kigeni kutoka kwenye miradi ya wawekezaji

Dola moja kwa sasa ni wastani wa Tsh. 2,300 mara ya mwisho kwa kiwango hicho kufikiwa ilikuwa ni Julai 2015 ambapo Benki Kuu ya Tanzania(BoT) iliingilia kati