Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 6:44 am

NEWS : BENKI KUU YA NCHINI LIBYA YADAI HALI YA UCHUMI NCHINI HUMO NI MBAYA

Benki Kuu ya Libya: Hali ya uchumi wa nchi ni mbaya

Gavana wa Benki Kuu ya Libya ametahadharisha kuhusu hali mbaya ya kiuchumi inayoikabili nchi hiyo.

Sadiq al Kabir ametahadharisha kuhusu hali mbaya ya kiuchumi ya Libya na kuwataka wabunge na serikali ya nchi hiyo kutekeleza majukumu yao kuhusu suala hilo.

Sadiq al Kabir, Gavana wa Benki Kuu ya Libya

Sadiq al Kabir amesema kuwa hazina ya Libya hadi sasa imepoteza dola bilioni 160. Gavana wa Benki Kuu ya Libya ameongeza kuwa kuzuiwa kusiko kwa uadilifu vyanzo vya mapato ya nchi hiyo kumesababisha nakisi ya bejeti ya uzalishaji jumla wa ndani kufikia kiwango cha asilimia 200.

Libya ilitumbukia katika mgogoro wa kisiasa na hali ya mchafukoge tangu kupinduliwa kiongozi wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi kufuatia uingiliaji kati kijeshi wa Marekani na waitifaki wake katika Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (Nato). Hali hiyo ya mchafukoge ilizusha mapigano kati ya Walibya na makundi ya kigaidi likiwemo kundi la Daesh.