- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BASI LA ABAIRIA LA SARATOGA LATEKETEA KWA MOTO
kIGOMA: Basi la kampuni ya Saratoga lililokuwa likitoka mkoani Kigoma kwenda Sumbawanga limepata moto na kuteketea lote katika eneo la kijiji cha Kazuramimba mkoani Kigoma asubuhi ya leo Agosti 20, 2018
Akizungumza na muakilishi.com kwa njia ya sim Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, ACP Martin Ottieno amesema kuwa jeshi lake bado linachunguza chanzo cha moto huo, ambapo amebainisha kuwa abiria wote sitini wamepona na baadhi ya mizigo imeokolewa.
“Gari limekaguliwa kabla ya kuondoka katika stendi ya mabasi kama kawaida ya utaratibu wa kikosi cha usalama barabarani na hakuna tatizo lililoonekana, hivyo chanzo cha moto huo bado hakija julikana tunafanya uchunguzi”, amesema Kamanda Ottieno.
Basi hilo limeungua ikiwa ni siku moja toka mtu mmoja kupoteza maisha katika ajali ya moto ulioteketeza malori katika mpaka wa Tanzania na Rwanda (Rusumo), baada ya gari la mafuta ya petrol kuligonga gari jingine na kupoteza mfumo wa breki.