- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BASHE ASEMA ANAWEZA KUONDOKA CCM KAMA LOWASSA
Dar es salaam: Mbunge machachali wa chama cha Mapinduzi CCM Hussein Bashe amesema anaweza kufata nyayo za Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa za kuondoka kwenye chama cha Mapinduzi iwapo chama hicho kitapoboronga
Amesema kuwa, anaweza kufanya hivyo kama alivyofanya viongozi wengine maarufu kama Maalim Seif Sharif Hamad na hata Augustino Mrema.
Akiongea leo Septemba 12, 2018 katika mkutano wa kampeni katika Jimbo la Ukonga wakati wa kumnadi mgombea wa chama hicho, Mwita Waitara, Bashe amesema kuwa, kuhama chama sio dhambi na kwamba alichokifanya Waitara ni haki yake kama walivyofanya wengine wakitoka CCM.
Mbunge huyo amepinga mitazamo ya wale wanaosema kuwa, Waitara alinunuliwana na CCM na kwamba, hoja hiyo ni dhaifu.
“Waitara namfahamu toka alipojuwa Umoja wa Vijana wa CCM-UVCCM” amesema Bashe na kuongeza:
“Aliondoka Mzee Augustine Mrema mwaka 1995, Maalim Seif naye akaondola hadi mzee wangu Lowassa alifanya hivyo, hatujawahi kutuhumu kama mtu amenunuliwa.
“Yoyote anapoamua kuwatumikia wananchi anapanda basi, vyama vya siasa ni sawa na basi, ukiona basi hilo dereva, kondakta hamuelewani unaweza kushuka kwenye basi hilo.”
Wakazi wa Jimbo la Ukonga wanatarajiwa kumchagua mbunge wao baada ya Waitara kujivua ubunge na kujiunga CCM ambayo imempitisha kugombea kwenye uchaguzi huo mdogo utaofanyika Jumapili ya Septemba 16 mwaka huu.
Jimbo lingine linalotarajiwa kufanyika uchaguzi siku hiyo ni Monduli pamoja na kata 22 nchini.