- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BASATA WAELEZEA MBINU ZA KUMBANA DIAMOND KUFANYA SHOW NJEE YA NCHI
Dar es salaam: Baraza la Sanaa la Tanzania BASATA limeeleza mbinu mbili kubwa itakayotumika kumbana msanii wa Bongo fleva Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz ikiwa ni pamoja na kumnyima kibali cha kufanya onesho au tamasha lolote njee ya nchi.
Basata walitangaza uamuzi wa kuwafungia siku ya jana Jumanne Diamond na Rayvanny wakisema hatua yao ilitokana na wawili hao kutofuata maagizo waliyopewa na baraza hilo wimbo wao wa Mwanza ulipopigwa marufuku Novemba.
Wasanii hao wawili walikuwa awali wametakiwa kuuondoa wimbo wao kwa jina 'Mwanza' kutoka kwenye mitandao ya kijamii, lakini wimbo huo umeendelea kuwepo kwenye YouTube na wamekuwa wakiucheza kwenye tamasha mbalimbali.
Kwa mujibu wa Afisa habari mkuu wa BASATA Bi Agnes Kimwaga amesema Baraza hilo lina mamlaka ya kumzuia msanii kutoka nje ya Tanzania.
"Kwa mujibu wa kanuni za Basata ya 2018, baraza linawajibika kumpa kibali msanii yeyote anapotoka nje ya nchi kwenda kufanya shughuli za sanaa. Kwa hivyo sisi ndio tutakaokutambulisha, na kibali hicho kitakuruhusu kuweza kutoka uwanja wa ndege kwenda kufanya shughuli yoyote ya sanaa nje ya nchi.
"Ikiwa tumekufungia kwa mujibu wa sheria, nani atakupatia kibali cha kukutambulisha kutoka nje ya mipaka ya nchi kwenda kufanya shughuli za sanaa.
"Kwa mujibu wa sheria tunaweza kumzuia kwenda kufanya nje ya nchi kwa sababu tutakataa kutoa vibali vya kumruhusu kutoka."
Bi Kimwaga amesema sababu ya kumfungia kwa muda usiojulikana ni kwa sababu inategemea kasi ya wahusika kutekeleza masharti waliyowekewa.
Miongoni mwa masharti hayo ni kulipa faini na kuuondoa wimbo huo kutoka kwenye mitandao ya kijamii.
Basata amesema kwa sasa bado ni mapema kuzungumzia uwezekano wa wanamuziki hao kupelekwa mahakamani iwapo wataendelea kukaidi maagizo ya baraza hilo.
"Itakuwa ni haraka sana kusema kwamba tunampeleka mahakamani. Basata ni walezi wa wasanii, na nina uhakika kama walezi mzazi yeyote mtoto anapokosea unajitahidi kwanza wewe kama mzazi kwa nafasi yako kujaribu kumrekebisha na kuhakikisha anafuata yale anayoyafanya. Tulikuwa na uhakika atafuata masharti."