- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BARUA YA KUJIUZULU YA KUBENEA YAZUA UTATA NDANI YA CHADEMA
Dar es salaam: Wakati chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wakipambana kutengeneza uwaminifu kwa wananchi baada ya kuathiriwa na kuhama hama kwa wabunge wake na Madiwani kumekuwepo na taharuki baada ya barua ya Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema), kuomba kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, jambo ambalo linaonekana kuleta mgongano na kurushiana mpira.
Lakini hadi sasa mbunge huyo wa Ubungo hajakubali wala kukataa kuhusu barua hiyo aliyomwandikia Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Vicent Mashinji ambaye anasema pindi itakapomfikia ataifanyia kazi haraka.
Barua hiyo ya Agosti 28 mwaka huu ilianza kusambaa mitaoni juzi, ambapo Kubenea alikuwa akitoa utetezi wake kutokana na kuandikiwa barua na na Katibu Mkuu wa chama hicho akitakiwa kujieleza kwanini asichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kusababisha migogoro kupitia mitandao ya kijamii.
Katika barua hiyo yenye kumbukumbu MB/U/CDM/018/1 kwenda Ofisi ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Kubenea alitakiwa kujibu tuhuma tano dhidi yake.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Dk. Mashinji alikiri kuona barua ya mbunge huyo kupitia mitandao ya kijamii, huku akiweka wazi kwamba pindi itakapomfikia ataifanyia kazi kwa haraka.
“Barua hiyo kama ambavyo umesema mwandishi ipo mitandaoni mimi bado sijaiona na kama nikiiona nitaifanyia kazi,’’alisema Dk. Mashinji.
Katika kile kinachooneka kuwa ni kukosekana kwa ufafanuzi wa kina Kubenea alikiri kupokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa chama hicho ikimtaka kujieleza kutokana na kikao cha Kamati Kuu (CC) iliyokutana Julai 7 na 8 mwaka huu.
Katika sehemu ya majibu ya Kubenea kwa Katibu Mkuu alieleza kukiri kupokea barua iliyoelekezwa kwake Julai 19 mwaka huu 2018 yenye Kumb. Na. C/HQ/K/PWN/MG/30/8, kuhusu “KUJIELEZA KWA KATIBU MKUU”