- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BANK KUU KUWAKAGUA WAFANYAKAZI WA MABENKI NCHINI
Dar es salaam: Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inatarajia kufanya uchambuzi na kuwakagua wafanyakazi wote wanaofanya kazi katika benki zote za hapa nchini.
Hayo yameelezwa na Gavana wa Benki Kuu Profesa Florens Luoga wakati akifunga semina ya waandishi wa habari za fedha na uchumi iliyoandaliwa na BoT Mjini Dodoma Profesa Luoga amesema uamuzi huo unalenga kulinda fedha za wananchi ambazo wameweka benki pamoja na kuondoa wafanyakazi wasio waaminifu.
"Benki Kuu tunao mkakati wa kuhakikisha tunafanya ukaguzi ambao lengo lake litakuwa kuhakikisha wanapatikana wafanyakazi waliowaamini na wenye uwezo wa kulinda fedha za wateja.Tunahitaji kuona wafanyakazi wa benki ambao wanatambua na kuheshimu misingi ya kaziza benki,"amesema Profesa Luoga na kuongeza ni muhimu kwa BoT kulinda za wateja.
Amefafanua siku za nyuma kulikuwa na baadhi ya fedha za wateja wadogo zilizohifadhiwa kwenye baadhi ya benki, ziliibwa kwa ujanja na wafanyakazi wa benki hizo jambo ambalo ni kinyume cha sheria. Ameongeza kiongozi mzuri wa benki lazima awe mwaminifu na ndio maana BoT wanataka kuhakiki wafanyakazi wa benki zote nchini.
Amefafanua huu ni wakati wa kuwa na wafanyakazi wa benki amabo ni sahihi kwa kazi hiyo, hivyo kupitia uchambuz wa kina ambao utafanyika watabaini wafanyakazi waliopo na uwezo wao na waamini kazini.
Profesa Luoga ameeleza namna ambavyo kuna baadhi ya wateja wa benki ambao si waaminifu walivyokuwa wanatengeneza mazingira ya kujipatia fedha ambapo walikuwa tayari kutafuta watu na kuwajazia fomu na kisha kuwapatia mkopo.
"Anakuja mfanyakazi wa benki fulani anakwambia fungua akaunti ili upate mkopo, baadae anakupa mkopo wa Sh.milioni 50 halafu yeye anachukua Sh.milioni 20 na kukuachia Sh.milioni 30.Lazima ifike wakati tuwe na wafanyakazi waamini katika sekta ya kibenki,"amesema. Amesema BoT imejipanga kwa kila hali kuhakikisha inalinda haki za wateja ikiwamo kulinda fedha zao kwenye benki huku akieleza kuwa wanataka huduma za kifedha zimfikie mwananchi kila mahali na bila kikwazo.