Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 9:34 am

NEWS: BALOZI WA CHAMA CHA CCM AKAMATWA NA GUNIA ZA BANGI

Watu wawili akiwemo Balozi wa nyumba kumi wakazi wa Kasumulu wilayani Kyela mkoa wa Mbeya, Andende Smoke Mbalwa (35) pamoja na Rose Charles (40) wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa tuhuma za kukutwa na debe tatu za bangi.

Kwamujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP, Ulrich Matei amesema watuhumiwa hao walinaswa katika operesheni iliyofanywa na jeshi hilo.

Kamanda Matei amedai kuwa, Mbalwa na Charles ni wauzaji na watumiaji wa bangi hiyo. Na kwamba upelelezi dhidi yao unaendelea na watafikishwa mahakamani mara baada ya kukamilika.

Katika hatua nyingie, Kamanda Matei amesema Polisi wanawashikilia watu watatu, Okoka Sanga (48) mkazi wa Ushirika Tukuyu, Festo Hassan (25) na Cosmas Ngondo (33) mkazi wa kijiji cha Lema wilayani Kyela, kwa tuhuma za kumjeruhi kwa kumchoma kisu sehemu za shingoni Elizabeth Mwampamba (44) mkazi wa Stamiko.

“Inadaiwa kuwa mnamo tarehe 1 Oktoba 2018 majira ya saa 00:05 usiku huko Kijiji cha Stamiko kilichopo Kata ya Busale, Tarafa ya Ntebela, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya. Elizabeth Mwampamba akiwa amelala nyumbani kwake ambapo anaishi na watoto wake, alivamiwa na mtu/watu wasiofahamika na kisha kuchomwa kisu sehemu za shingoni,” amesema Kamanda Matei.

Kamanda Matei amesema Mhanga wa tukio hilo amelazwa Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa matibabu. Wakati polisi wakiendelea na upelelezi kubaini chanzo cha tukio hilo.