November 28, 2024, 11:44 pm
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BABA ATIWA MBARONI KWA KUMBAKA MWANAE WA MIAKA 12
SERENGETI: Mkazi wa Stendimpya, Mugumu, Nyamhura Werema (35)amepandishwa Mahakama ya Wilaya ya Serengeti kwa kosa la kumbaka mtoto wake wa miaka(12).
Akizungumza mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Ismael Ngaile, mwendesha mashtaka wa polisi, Paskael Nkenyenge amesema kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Julai mwaka huu.
“Mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 158(1) (a) cha kanuni ya adhabu sura 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002,” amesema
Amesema Upelelezi haujakamilika na mshitakiwa amekana shitaka. Mshtakiwa amenyimwa dhamana na kesi yake itatajwa tena Septemba mwaka huu.
Newest Posts