- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BAADA YA WAZIRI MKUU KUJIUZULU RAIS WA MALI AUNDA SERIKALI MPYA
Rais wa Mali aunda serikali mpya baada ya Waziri Mkuu kujiuzulu
Rais Ibrahim Boubacar Keita ametangaza kuunda serikali mpya, masaa machache baada ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo kutangaza kujiuzulu ghafla pamoja na baraza lake la mawaziri.
Kwa mujibu wa dikrii iliyochapichwa jana Jumapili, Rais Keita amemteua mpambe wake wa karibu Soumeylou Boubeye Maiga kujaza nafasi ya Waziri Mkuu aliyejiuzulu siku ya Ijumaa, Abdoulaye Idrissa Maiga, huku akiwateua mawaziri wapya sita.
Kadhalika amemteua aliyekuwa Waziri wa Utawala wa Kieneo, Tieman Hubert Coulibaly kujaza nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje, Abdoulaye Diop.
Hii ni serikali ya tano kuundwa na Rais Keita tangu alipochaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika Agosti mwaka 2013.
Keita anakabiliwa na changamoto za kiusalama katika maeneo ya kaskazini na katikati mwa nchi hiyo.
Mwaka 2013 yaani baada ya wanajeshi wa Ufaransa kuingia nchini Mali, makundi yenye misimamo mikali yalipata kisingizio cha kujikusanya upya na kuanzia wakati huo hadi hivi sasa yamekuwa yakiwashambulia mara kwa mara askari wa kigeni na wa serikali katika maeneo ya kaskazini na katikati mwa nchi hiyo.