Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 5:39 am

NEWS : BAADA YA ASKARI WA UN KESHINDWA UN YAANZA UCHUNGUZI WA MADAI HAYO

UN yaanza uchunguzi wa madai ya kufeli askari wa kimataifa huko CAR

UN yaanza uchunguzi wa madai ya kufeli askari wa kimataifa huko CAR

Umoja wa Mataifa umenzisha uchunguzi juu ya madai ya kufeli kwa kikosi cha askari wa kimataifa wa kulinda amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR).

Kitengo cha Opresheni za Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa kimetangaza kuwa, kimenzisha uchunguzi wa kubaini ukweli kuhusu madai kwamba askari wa umoja huo wanaolinda amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wameshindwa kutekeleza majukumu

Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Mataifa imesema kuwa, kundi la wataalamu limepewa jukumu la kuchunguza matukio yaliyojiri kusini mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati mwezi Agosti mwaka huu.

Askari wa UN Jamhuri ya Afrika ya KatI

Wataalamu hao watachunguza mashambulizi yaliyofanywa na wanamgambo dhidi ya raia waliokuwa karibu na kambi ya askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na kutaka kujua iwapo askari hao walichukua hatua yoyote ya kuzuia mashambulizi hayo ya waasi ao la.

Uchunguzi kuhusu utendaji wa askari wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati unafanyika wakati Baraza la Usalama la umoja huo limetakiwa kurefusha muda wa kazi za kikosi hicho na idadi ya wapiganaji wake.