- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : ATWAN : ISRAEL HAINA UBAVU WA KUTEKELEZA VITISHO WANAVYOVITOA IRAN
Atwan: Israel haina ubavu wa kutekeleza vitisho inavyotoa dhidi ya Iran
Gazeti la Al-Ra'yul-Yaum limeandika kuhusu vitisho hewa vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kueleza kwamba Tel Aviv haiwezi kutekeleza kivitendo vitisho vyake vya kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Iran nchini Syria na kumuua kigaidi Jenerali Qassim Soleimani, kwa sababu ikijaribu kufanya hivyo itakabiliwa na mwisho mbaya na si hasha ikawa sababu ya kuangamizwa moja kwa moja.
Katika makala iliyoandikwa na Abdel Bari Atwan kwenye toleo la jana Jumanne la gazeti hilo, Al-Ra'yul-Yaum limeongeza kuwa, katika siku tatu zilizopita Israel imetoa vitisho viwili hatari ambavyo haidhaniwi kama itakuwa na uthubutu wa kutekeleza kitisho hata kimoja kati ya viwli hivyo kwa sababu inaelewa fika kwamba, itavilipia gharama kubwa na si hasha vikahitimisha uwepo wake.
Abdel Bari Atwan amefafanua katika makala yake hiyo kwamba, Iran haina haja ya kuweka vituo vya kijeshi nchini Syria na kama itahitaji kufanya hivyo haitoshughulishwa na vitisho kama hivyo na kuongeza kuwa, Iran ipo kijeshi kisheria nchini Syria kwa sababu inafanya hivyo kwa ridhaa ya serikali halali ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa Atwan, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Benjamin Netanyahu ana hofu ya kupanuka muungano wa Iran na Syria kwa uungaji mkono wa vikosi vya harakati ya Hizbullah ya Lebanon na anahisi muungano huo ni tishio la kistratijia kwa usalama wa Israel.
Ameongeza kuwa utawala wa Kizayuni una hofu ya vitisho vya Iran dhidi ya uhai wa utawala huo bandia, kama ambavyo una wasiwasi pia kutokana na kuongezeka nguvu za kijeshi na kisiasa za Hizbullah na uhusiano wa muungano imara uliopo baina yake na harakati za Hamas na Jihadul-Islami katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu