Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 11:28 am

NEWS: ATOA AGIZO KUUNDWA KWA BODI YA WANAJIOLOJIA

Dodoma: Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani ametoa Agizo kuwa wataalamu wote wanaohusika na uundwaji wa bodi ya wanajiolojia nchini kuanza mchakato huo mara moja ili bodi hiyo iundwe haraka.

Kalemani ametoa agizo hilo leo Oktoba 1 wakati akifunga kikao kilichowakutanisha wanajiolojia nchini.

Dk Kalemani amesema uundwaji wa bodi hiyo utaleta ufanisi wa kazi kwa wanajiolojia hao na kuongeza ajira kwa Watanzania kwa kuwa wengi

wao kwa sasa hawana ajira.

“Nawaagiza wanaohusika na uundwaji wa bodi waanze taratibu za uundwaji wa bodi hiyo,” amesema Dk Kalemani.

Amesema kuwa bodi hiyo itakaposajiliwa itawaajiri Watanzania wengi na pia watatambulika rasmi kwa kutumia taaluma yao ambayo kwa

sasa haitambuliki kwa kuwa hakuna bodi inayowaunganisha.

“Bodi hiyo ikiundwa hata wataalamu kutoka nje wakitaka kuja kufanya kazi zao hapa nchini ni lazima watapitia kwenye bodi na huko lazima watawatumia Watanzania katika kazi zao ambapo nao watapata

ajira,” amesema Dk Kalemani na kuongeza kuwa,

“Kwa kutokuwa na bodi hii kumechelewesha sana ajira za Watanzania wenye tasnia hii.”

Bodi hiyo ya wanajiolojia nchini inaundwa kufuatia maagizo ya Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa alilolitoa wakati akifungua mkutano wa wanajiolojia Septemba 27 mwaka huu.

Akizungumza katika mkutano huo, Naibu Waziri wa Madini, Stansilaus Nyongo amesema nchi ina utajiri mkubwa wa madini pamoja na wataalamu wa jiolojia waliobobea kwa hiyo kwa kutumia Serikali makini

madini hayo yanaweza kuwatajirisha Watanzania walio wengi.