- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ASKOFU MKUU KANISA KATOLIKI JIMBO LA MBEYA AMEFARIKI DUNIA
Dar es Salaam: Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Mbeya, Evarist Chengula amefariki dunia Mchana wa Leo Novemba 21 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika Hosptali ya Muhimbili Jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Dk Charles Kitima amesema Askofu Chengula alifariki leo Jumatano akiwa anapatiwa matibabu ya moyo.
“Ni kweli askofu wa jimbo la Mbeya baba Chengula amefariki leo saa tatu asubuhi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Muhimbili,’’ amesema.
Amesema kuwa askofu Chengula alikuwa anasumbuliwa na tatizo la moyo na aliwasili Muhimbili jana Jumanne (Novemba 20, 2018) akitokea mkoani Mbeya.
‘Si kuwa alikuwa mgonjwa sana, alikuwa na tatizo la moyo lakini juzi alikuwa ametoka kazini huko vijijini likaanza kumzidia, sasa jana (Jumanne) akaamua aje hospitalini,’ amesema Dk Kitima
Askofu huyu alitolea ufafanuzi ujumbe uliotolewa na maaskofu wakatoliki akisema ujumbe ulikuwa haumlengi mtu fulani bali uliwalenga wanafiki wanaodai ni Wakristo lakini hawana imani ya Kikristo ili waweze kubadilika na kuwa watu wema.