- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ASKOFU AWATETEA MASHOGA ATAKA WASITENGWE
Bukoba: Taarifa kubwa kutoka Mkoani Kagera zimeripoti kuwa Askofu mkuu wa Jimbo la kiKatoliki la Bukoba mkoa humo Desiderius Rwoma amekemea vitendo vya ushoga lakini akawataka wanaofanya dhambi kama hiyo wasitengwe na kubaguliwa na jamii na badala yake wasaidiwe na kuonyeshwa ubaya wa wanachofanya.
Askofu Rwoma amesema kumvumilia mkosefu yeyote haina maana ya kumuunga mkono na kuwa ushoga ni dhambi na laana na watu wenye tabia hiyo wanahitaji msaada wa matibabu na huduma za kisaikolojia na sio kuwatenga.
Katika mahubiri yake leo katika siku ya wanaume wa Jimbo Katoliki kwenye kanisa la Bikra Maria Mama wa Huruma, Askofu Rwoma ametaka uwepo wa sheria za kudhibiti vitendo vya ushoga nchini.