Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 1:30 am

NEWS: ASKARI ALIYEMUUWA MPENZI WAKE AJISALIMISHA KITUONI AKIWA NA MAJERAHA

NJOMBE: Askari wa Jeshi la Polisi kwa jina Zakayo Dotto anayetuhumiwa kumuua kwa kumpiga risasi Askari wa Kike Neema Masanja wa JWTZ ambaye alikuwa ni mpenzi wake, ajisalimisha Polisi leo asubuhi baada ya kutoroka siku ya jana - Akutwa na majeraha yanayoashiria jaribio la kujidhuru,

Jana Askari huyo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kikosi cha Makambako (KJ 514) ambaye amefahamika kwa jina la Neema Masanja amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na mchumba wake Zakayo Dotto ambaye ni askari wa Jeshi la Polisi Makambako mkoani Njombe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Prudensiana Protas alidhibitisha kutokea kwa tukio hilo mapema jana na kusema kuwa Askari wa jeshi la polisi Makambako mkoani Njombe ambaye anafahamika kwa jina la Zakayo Dotto alifanya tukio hilo la mauaji kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.