- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ASKARI 4 MBARONI KWA KUPOKEA RUSHWA
Kiteto. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) inawashikilia Askari wanne wa pori la akiba la Mkungunero Wilaya ya Kondoa Mkoa wa Dodoma wakituhumiwa kuomba na kupokea rushwa ya Sh5 milioni za wafugaji wa Kijiji cha Irkiushiboir Kata ya Makame Wilaya ya Kiteto mkoani Mnyara.
Akizungumza leo May 22 kamanda wa TAKUKURU wilayani kiteto mkoani manyara ndugu. Julius Chacha amesema ni kweli askari hao wamekamatwa toka juzi May 20 wakiwa na Bunduki 4 zote za SMG huku wakiwa na mifugo 200.
Amewataja askari hao kuwa ni Godfrey Matheas, Martenus Mahoka, Augustino Sadiki na Aphrahimu Polepole. Amebainisha kuwa baada ya mmoja wa wafugaji kuombwa rushwa na watu hao, uliwekwa mtego na kukamatwa askari hao wakiwa wamepokea kiasi hicho cha fedha na kwamba walikuwa na mifugo zaidi ya 200 mali ya familia saba za wilayani Kiteto. “Mtego huo uliwekwa kabla ya askari hao kuikabidhi mifugo kwa wenyewe.
Tuliwakamata wahusika wakiwa wameshikilia mifugo hiyo katika kitongoji cha Ilchura kijiji cha Irkiushiboir wilayani Kiteto,"amesema Chacha.