- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: APIGWA RISASI NA KUFARIKI NDUNIA BAADA YA KURUKA UZIO WA JESHI JWTZ
PWANI: Mwanaume mmoja jina lake halikuweza kufahamika amefarika Dunia baada ya kupingwa Risasi na Jeshi la JWTZ baada ya kukimbia na kukaidi amri ya kusimama alipoingia kwenye kambi ya jeshi kinyume cha utaratibu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, leo Jioni Wankyo Nyigesa, amesema mtu huyo aliingia kwenye Kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) kwenye kambi iitwayo Mapinga Comprehensive Training Centre (CTC).
Kamanda Nyigesa alisema kuwa tukio hilo lilitokea leo Jioni Septemba 11, muda wa saa 9 kwenye kambi hiyo iliyopo Mapinga wilaya ya Bagamoyo ambapo aliingia kwa kuruka ukuta. “Mwanamume huyo baada ya kuingia, walinzi wa JWTZ ambao walikuwa zamu walimwamuru asimame lakini aliendelea kukimbia pia walirusha risasi hewani ili asimame lakini alikaidi na kuzidi kukimbia ndipo walimfyatulia risasi iliyompata kiunoni,” alisema Nyigesa.
Alisema kuwa baada ya kufyatuliwa risasi hiyo alidondoka chini na kuanza kuvuja damu na alifariki dunia akiwa njiani kupelekwa hospitali kutokana na damu nyingi kuvuja. “Tunatoa mwito kwa wananchi kuacha kuingia kwenye maeneo ya jeshi na yale ya hifadhi yenye ulinzi wa askari pasipo kufuata taratibu za kisheria ya kuingia kwenye maeneo hayo,” alisema Nyigesa.
Aidha alitoa rai kwa wananchi pale wanapokuwa wameingia kwenye maeneo hayo ni vema kuwa watiifu wanapotakiwa kusimama ili kuweza kuhojiwa na kuelekezwa iwapo watakuwa wameingia kwenye maeneo hayo kimakosa. “Ifahamike kuwa maeneo yote yenye ulinzi wa askari yana taratibu zake ambazo zinapaswa kuheshimiwa na kila mmoja wetu jambo ambalo mtu huyo angekuwa amezifuata taratibu hizo basi pasingeweza kutokea madhara hayo,” alisema Nyigesa.