- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ANG'OLEWA MADARAKA KWA KUMBAKA MWANAFUNZI.
“Imebainika hili ni tukio la nne kwa mwalimu huyo kutuhumiwa kufanya mapenzi na wanafunzi tofauti tofauti lakini amekuwa hachukuliwi hatua, lakini mimi kwa mujibu wa sheria nimemvua madaraka mwalimu mkuu huyo ili awe mwalimu wa kawaida, sababu amekosa maadili ya kuendelea kushika wadhifa huo,” alisema mkurugenzi huyo.
Aidha, alisema kesi hiyo tayari imefikishwa polisi na wakati wowote mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani. Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga alisikitishwa na kitendo hicho na kumtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo kumchukulia hatua na kuwashauri wazazi wamuache mwanafunzi huyo aendelee na masomo yasije yakampita huku hatua za kisheria kwa mtuhumiwa zikiendelea.
Mlezi wa mwanafunzi huyo, alisema mwanawe alisimama masomo kwa muda wa wiki mbili kutokana na tukio hilo. Mwalimu Ng’waya alipozungumza na mwandishi wa habari kwa njia ya simu alikiri kuvuliwa madaraka na kueleza amekuwa mwalimu wa kawaida huku akiendelea kufundisha katika shule hiyo