- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ALIYEMUHONGA WAZIRI LUKUVI MILIONI 90 AACHILIWA HURU
Dar es salaam: Mahakama ya Wilaya ya Ilala hatimaye imemuachia huru, Mohamed Kiluwa (50) aliyekuwa akikabiliwa na shtaka la kutoa rushwa ya Sh milioni 90 kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kwa sababu ushahidi wa mashtaka ulikuwa wa hisia.
Akisoma hukumu hiyo leo Jumatatu Desemba 24, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo Samuel Obas amesema ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka haukuwa na mashiko kwa sababu umeshindwa kuthibitisha kosa.
Amesema kutokana na hali hiyo, mahakama hiyo imemuachia huru na kuamuru fedha zake ambazo ni Sh milioni 90 arudishiwe.
Hata hivyo, ameruhusu upande wa jamhuri kukata rufaa kama hawajaridhika na uamuzi huo.