- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ALIYEKUWA RC DOM: 'NITAENDELEA KUWA RAIA MWAMINIFU'
DODOMA: Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jodarn Rugimbana amesema kuwa licha ya kuwa Rais Dkt. John Magufuli amemuondoa katika nafasi hiyo lakini bado ataendelea kuwa raia mwaminifu na timu Magufuli wakati wote ili kuhakikisha malengo ya serikali ya awamu ya yanatimia.
Rugimbana ametoa kauli hiyo mjini hapa leo wakati wa hafla ya makabidhiano ya Ofisa Kati yake na mkuu mpya wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilithi Mahenge.
Makabidhiano hayo yamefanyika kufuatia mabadiliko ya viongozi wakiwemo wakuu wa mikoa yaliyofanywa wiki iliyopita na Rais, John Magufuli ambapo Rugimbana ni miongoni mwa wakuu wa mkoa walioachwa katika uteuzi huo
Hata hivyo rugimbana hakusita kuzungumzia mchakato wa serikali kuhamia Dodoma chini ya usimamizi wa Ofisi ya waziri mkuu, akisema kuwa ni jambo lililochukua takribani miaka 40.
Naye mkuu mpya wa Mkoa wa Dodoma, Dk.Mahenge amesema, atamuenzi Rugimbana kwa kusimamia na kuyafuatilia mambo yote yaliyofanywa kwa kuwa no ni maelekezo ya timu aliyokuwa akifanya kazi nayo huku akiomba ushirikano kwa watumishi na wananchi wa dodoma kwa ujumla.