Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 11:28 pm

NEWS: ALIYEKUWA MBUNGE WA CCM ASEMA CCM WANASHINDA KWA WIZI WA KURA

Aleyewahi kuwa Naibu Wazari wa Kazi na Ajira Makongoro Mahanga amesema nyakati ambazo anagombea akiwa na chama cha mapinduzi CCM alishinda ubunge kutokana na wizi wa kura unaofanywa na chama chake cha zamani.

Mahanga ambae pia ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Ilala, amewahi kuwa mbunge wa Jimbo la Ukonga kwa miaka kumi kuanzia 2000 mpaka 2010 na baadaye jimbo hilo liligawanywa na kuzaliwa Segerea ambako naibu waziri huyo wa zamani aliliongoza kuanzia mwaka 2010 mpaka 2015.

Akizungumza jana Agosti 25 wakati wa uzinduzi wa kampeni za ubunge wa Jimbo la Ukonga, Mahanga ambaye alihamia Chadema siku chache kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 alisema aliongoza Jimbo la Ukonga kwa miaka 10 na sababu kubwa iliyomfanya ashinde ni kununua kura na hivyo akawataka wananchi wasikubali kununuliwa. “CCM nawafahamu sana, wanawatumia mabalozi kununua kadi za kupigia kura hata mimi walikuwa wananifanyia hivyo na ninashinda,” alisema Mahanga bila kuwa na nyaraka za kuthibitisha kuhusu madai hayo.

“Kura zinazoibiwa sio za Chadema ni za wananchi, wananchi kataeni kuibiwa,”alisema. Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa CCM, Kanali Ngemela Lubinga ambaye alisema yupo safarini Mkoa wa Lindi hakusita kumjibu Mahanga jana. Lubinga alisema Dk Mahanga ni mtu wa kupuuzwa kwani anadhalilisha elimu aliyonayo. “Huwezi ku-deal na mtu kama huyo. Yaani anawaambia wananchi kuwa alikuwa anaiba kura? ili iweje? Anaidhalilisha hata PhD (shahada ya uzamivu) aliyonayo tu, kama huyo ni wa kuachana naye,” alisema Lubinga. Uchaguzi huo mdogo utafanyika Septemba 16 baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Mwita Waitara kujiuzulu uanachama wa Chadema na kuhamia CCM. CCM wamemteua Waitara kuwania jimbo hilo na Chadema wamemteua Asia Msangi.