- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ALICHOKIZUNGUMZA MGOMBEA WA CHADEMA UKONGA BAADA YA KUSHINDWA
Dar es Salaam: Aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Ukonga kwa tiketi ya Chadema, Asia Msangi amesema hajashangazwa na matokeo ya uchaguzi wa jimbo hilo kwa kuwa dalili zilianza kuonekana mapema tokea jana alfajiri.
Akizungumza leo Septemba 17, 2018 Msangi amesema kitendo cha mawakala kuzuiwa kuingia vituoni na mazingira yaliyozunguka uchaguzi huo yalihalalisha ukandamizwaji wa demokrasia.
Amesema dalili za kuangushwa kwake zilianza kuonekana saa mbili asubuhi kutokana na mchezo mchafu uliofanywa ili asishinde.
“Maisha yanaendelea, nawashukuru sana wakazi wa Ukonga wameonyesha kunikubali mno ila mazingira yaliyopo ni kama walivyojionea. Niwape pole kwa yote yaliyotokea tuache kila jambo lina mwisho wake,” amesema.
“Nawasihi wasife moyo tutafanya kazi kwa kuwa yale yote niliyokuwa nikiwaambia yapo kwenye fremu ya kichwa changu tutashirikiana kuyafanyia kazi kwa kuwa na mimi ni mkazi wa Ukonga,”
Kuhusu hatua zipi zitafuata Msangi amesema, “Bado nipo na wanasheria wangu na viongozi wangu wa chama tunaendelea kujadiliana, tukifikia uamuzi tutawataarifu kwa sasa ni mapema mno kutoa msimamo wa chama.”
Katika uchaguzi uliofanyika jana Septemba 16, Tume ya uchaguzi ilimtangaza mgombea wa CCM, Mwita Waitara kuibuka mshindi na kuendelea kulitumikia jimbo hilo.
Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo la Ukonga Jumanne Shauri alimtangaza Waitara kuwa mshindi kwa kura 77,795 sawa na asilimia 89.19 na Msangi alipata kura 8676 sawa na asilimia 9.95.
Watu waliotarajiwa kupiga kura ni 300,609 ila waliojitokeza ni 88270 sawa na asilimia 29.4