- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: AL BASHIRI AMTEMBELEA RAIS WA URUSI, LICHA YA ICC KUMUHITAJI
Rais wa Sudan Omar al-Bashir Leo Novemba 23 anakwenda nchini Urusi kwa ziara ya kibiashara.Al Bashir anafanya ziara yake ya kwanza rasmi nje ya nchi tangu nchi yake kufutiwa vikwazo na Marekani. Atapokelewa katika ikulu ya Kremlin na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin.
Taarifa hii ilitolewa na mamlaka ya Sudan na kuthibitishwa mapema wiki hii na ikulu ya Kremlin. Omar al-Bashir anatarajiwa Alhamisi hii mjini Moscow na anapaswa kukutana kwa mazungumzo na rais wa Urusi.
Mikataba ya ushirikiano inaweza kusainiwa pamoja na mikataba katika sekta ya madini, kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Sudan.
Ziara hii ambayo ilipangwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu, itakua ni ziara ya kwanza ya Omar al-Bashir nchini Urusi.
Licha ya waranti mbili za kukamatwa zilizotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) dhidi yake, hakuna uwezekano wowote wa rais Bashiri kukamatwa na polisi wa Urusi. Russia haijawahi kusaini Sheria ya Roma inayounda Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu.
Aidha, Moscow ilifuta saini yake kwenye Sheria ya Roma mnamo mwezi Novemba 2016 kufuatia ufunguzi wa uchunguzi wa vita vya mwaka 2008 kati ya Urusi na Georgia. Hatimaye, Vladimir Putin anatarajia kuendeleza uhusiano wa biashara na kisiasa kati ya nchi yake na Sudan.