- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: AKAMATWA KWA KUWABAKA WANAWAKE KWA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA
MWANZA: mkazi wa Mwanza, Kenned Obworo (35), amekamatwa na Jeshi la polisi akituhumiwa kuwanywesha dawa za kulevya wanawake na kisha kuwabaka na kuwaibia mali zao.
kwa mujibu wa Kamanda Shana alisema Jumatano iliyopita, saa mbili usiku katika Hoteli ya Haven iliyopo Nyasaka, Ilemela alimchukua mwanamke mmoja na kumnunulia Red Bull kisha akamuwekea dawa hizo na baada ya kulewa alimuingiza chumbani na kumbaka. Alisema tukio kama hilo lilitokea Magu Jumatatu iliyopita katika baa iitwayo Dear Sija Lodge.
''amekuwa akiwalaghai wanawake kwa kuwanunulia chakula na vinywaji kisha kuwawekea dawa zinazodhaniwa kuwa ni za kulevya ili awabake, kuwaibia fedha na simu za mkononi, kazi ambayo anadaiwa kuifanya kwenye nyumba za wageni ambazo anakuwa amekodisha. Kamanda Shana alisema Jumatano iliyopita, saa mbili usiku katika Hoteli ya Haven iliyopo Nyasaka, Ilemela alimchukua mwanamke mmoja na kumnunulia Red Bull kisha akamuwekea dawa hizo na baada ya kulewa alimuingiza chumbani na kumbaka''
Alisema tukio kama hilo lilitokea Magu Jumatatu iliyopita katika baa iitwayo Dear Sija Lodge. Alisema kabla ya tukio hilo, wanawake wanne walikutana na mtuhumiwa huyo katika baa ya Villa Park, Mwanza ambao walimuomba awanunulie vinywaji. Alifanya hivyo kisha wakapeana namba za simu na kuachana salama. Alisema wanawake wawili kati ya wanne, walimpigia simu wakakubaliana wakutane tena Villa Park na walipokutana waliafikiana waende Kisesa kwa kutumia gari la mmoja wa wanawake hao. Baada ya kufika Dear Sija, Kamanda Shanna alisema waliagiza vinywaji kisha wanaume wawili akiwamo mtuhumiwa waliingia chumbani na kuwaingiza wanawake hao ambao waliwalevya na kuwabaka kisha kuwaibia simu mbili za Sumsung na kuwaacha hawajitambui. Alisema baada ya kufanya upekuzi kwenye vyumba hivyo walikuta vidonge aina ya Lorenzepam na mtuhumiwa amekiri kufanya matukio kama hayo katika mikoa ya Dar es Salaam, Geita, Mara, Arusha na Mwanza.