- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: AJIPIGA RISASI BAADA YA KUMJAZA MWANAFUNZI MIMBA
Serengeti: Askari mmoja aliyekuwa na cheo cha sajenti katika Gereza la Mradi Tabora B, alijiua kwa kujipiga risasi mbili mdomoni nyumbani kwake juzi Novemba 9 na kabla ya kujiua, aliacha ujumbe wa maandishi ukisema alijiua kutokana na kuumwa tumbo kwa muda mrefu.
Kifo cha Askari huyo kimeleta mshtuko kwa familia moja ya Mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Kisangura wilayani humo, wakisema kujiua kwa askari Magereza, huyo muda mfupi baada ya kutajwa kumpa mimba mtoto wao, kumewachanganya Sana
Lakini Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Juma Ndaki juzi alisema kuwa Tangawizi alikuwa amefunguliwa jalada katika kituo cha polisi akituhumiwa kumpa mimba mwanafunzi wa sekondari.
“Kwa sasa kama familia, hatujui tufanye nini maana aliyetajwa na mwanangu kuwa alimpa mimba inaonekana alipewa taarifa na polisi na kuchukua uamuzi huo mgumu, ingawa ujumbe alioacha ni tofauti na tukio, hili limetuchanganya,” alisema Joseph baba wa mtoto huyo.
Joseph ambaye ni kiongozi wa kikundi cha Kwiyengo cha Kanisa la Wasabato Bonchugu, Kata ya Sedeko alisema hakuwa na taarifa kama mwanaye ana ujauzito wa miezi minne hadi alipoitwa na kuelezwa na mkuu wa shule Novemba 5.
“Nilipofika niliambiwa kuhusu suala hilo sikuamini, niliamua kumchukua mwenyewe na kumpeleka Zahanati ya Bonchugu, akapimwa na tarehe sita nikafuata majibu ndipo ikabainika kuwa ni mjamzito, mbele ya mwalimu alimtaja aliyempa mimba na kutoa namba ya simu waliyokuwa wakiwasiliana naye,” alisema.