- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: AJALI YAUWA WATATU WA FAMILIA MOJA MKOANI DOM
DOM: Watu Wanne Wamefariki Dunia Wakiwemo Watatu Wa Familia Moja Katika Ajali Mbili Tofauti Huku Wengine Watatu Wakijeruhiwa Katika Barabara Kuu Ya Singida Dodoma.
Akizungumza Akiwa Katika Eneo La Tukio Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi Wa Polisi Gilles Muroto Amethibitisha Kutokea Kwa Ajali Hiyo Ambapo Amesema Matukio Ya Ajali Yamekuwa Yakipoteza Nguvu Kazi Ya Nchi Na Kuwataka Watumiaji Wa Vyombo Vya Usafiri Kuzingatia Sheria Za Usalama Barabarani Ili Kuepuka Ajali Za Barabarani
‘’Chanzo Cha Ajali Hiyo Ni Uzembe Wa Bodaboda Kushindwa Kuchukua Tahadhari Wakati Akiingia Barabara Kuu’’
Aidha Katika Hatua Nyingine Kamanda Muroto Amesema Ajali Nyingine Imetokea Katika Eneo La Kizota Jijini Dodoma Na Kuhusisha Maroli Mawili Na Gari Ndogo Na Kusababisha Majeruhi Wawili Ambapo Amesema Jeshi La Polisi Mkoa Wa Dodoma Linaendelea Kutoa Elimu Kwa Madereva Ili Kutii Sheria Za Usalama Barabarani
Muakilishi News Imefika Katika Hospitali Ya Rufaa Ya Mkoa Wa Dodoma Na Kuzungumza Na Kaimu Mganga Mfawidhi Wa Hospitali Ya Rufaa Ya Mkoa Wa Dodoma Dr Mnzava David Ambapo Hapa Anaeleze Hali Za Majeruhi.
Wakizungumza Na Muakilishi news Baadhi Ya Mashuhuda Wamesema Kuwa Chanzo Cha Ajali Hizo Ni Uzembe Wa Madereva Kutozingatia Alama Za Usalama Barabarani Huku Wakiwataka Madereva Kutii Sheria Za Usalama Barabarani Ambapo Wananchi Hao Wameonyesha Kusikitishwa Na Ajali Ambazo Zimekuwa Zikigharimu Maisha Ya Watu