Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 11:32 pm

NEWS: AHUKUMIWA BAADA YA KUMKATA KIDOLE MKEWE

Dodoma: Mwanaume mmoja kwajina Jeva Msusu 43, Mkazi wa kijiji cha Chogola wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma amehukumiwa kifungu cha maisha Jela na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani humo baada ya kumfanyia ukatili mke wake kwa kumkata kidole chake cha mkono wa kushoto na kukiondoa kabisa.

Kesi hiyo ilikuwa inasikilizwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpwawa, Pascal Mayumba.

Hakimu Mayumba aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa kinyume na kifungo cha Sheria Namba 222 kifungu kidogo (a) na (b) ya kanuni ya adhabu iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Pia Mayumba aliiambia mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa huyo bila halali yoyote alimjeruhi, Pendo Charles ambae ni mke wake kwa kumkata kidole chake na kukiondoa.

Akisomewa hoja za awali na Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Willison Mwita, mtuhumiwa huyo alikiri hoja zote na mahakama haikuwa na hoja zilizopingwa.

Ndipo hakimu Mayumba akamuhukumu kifungo cha maisha jela.