- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: AFRIKA KUSINI YAHALALISHA MATUMIZI YA BANGI
Nchi ya Afrika kusini kupitia Mahakama ya Kikatiba nchini humo imehalalisha utumiaji wa bangi kwa watu wazima katika maeneo ya faragha.
Majaji wote kwa pamoja kupitia Mahakama hiyo walifikia uamuzi huo kwa kauli moja, kuruhusu watu wazima kutumia bangi wakiwa majumbani na kukuza kiasi kinachoweza kutosheleza mahitaji binafsi.
Imekuwa ni ushindi kwa Wanaharakati nchini humo wanaounga mkono utumiaji wa bangi na kuwafanya kusheherekea uamuzi huo wa kihistoria wakisema ''sasa tuko huru''.
Pia Baraza la ukuzaji bangi nchini Afrika Kusini limeunga mkono uamuzi wa mahahakama dhidi ya matumizi ya bangi na kutoa wito kwa serikali kuwaondolea mashtaka watu waliyopatikana na kileo hicho.
Akitoa hukumu hiyo Naibu jaji Mkuu, wa Afrika Kusini, Raymond Zondo, amesema sheria inayopiga marufuku watu wazima kutumia bangi ilikuwa kinyume cha katiba.
Serikali ya Afrika kusini bado haijatoa tamko lolote kuhusiana na na uamuzi huo.
Watumiaji watatu wa bangi walikuwa wanakabiliwa na mashtaka walijitetea mbele ya mahakama hiyo wakisema '' mashataka dhidi yao yaliingilia uhuru wao''
Naibu jaji mkuu Raymond Zondo alisema: "Sio hatia kwa mtu mzima kutumia au kugusa bangi akiwa katika eneo la faraghani hasa ikiwa anafanya hivyo kwa maatumizi yake ya kibinafsi''
Licha ya uamuzi huo, ni hatia kwa mtu kuvuta au kuuza bangi hadharani.