- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: AFISA USALAMA FEKI APEWA SIKU 2 NA DC KUJISALIMISHA
Mwanga: Mkuu wa wilaya ya Mwanga, Aaron Mbogho, amempa siku 2 sawa na saa 48 kwa mtu mmoja anayejifanya ni ofisa wa Usalama wa Taifa na kuwatapeli wavuvi katika bwawa la Nyumba ya Mungu kujisalimisha polisi mara moja kabla ya kazi ya kipolisi haijaanza kumsaka.
Mbogho ametoa agizo hilo jana Desemba 9,2018 katika kijiji cha Lang’ata Bora, alipokwenda kwa ajili ya kazi ya kuteketeza zana za uvuvi haramu zilizokamatwa kijijini hapo.
Agizo la Mbogho linatokana na malalamiko ya wananchi kuwa mtu huyo amekusanya fedha kwa wavuvi akisema anazipeleka kwa mkuu huyo wa wilaya ili kulegeza operesheni dhidi ya uvuvi haramu.
Wavuvi katika kijiji hicho walimweleza mkuu wa wilaya kuwa mtu huyo anayejiita Sajo alichukua fedha hizo akidai anazipeleka kwake ili awaruhusu kuvua katika mwalo mdogo uliozuiwa.