Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 1:44 am

NEWS: AFISA MISITU DOM ALAANI KITENDO CHA UKATAJI WA MITI OVYO

DODOMA: Afisa misitu wa manispaa ya Dodoma Alexanda Kabado amewataka wananchi kuacha tabia ya ukataji wa Misitu ovyo ili kupunguza ukame katika Mkoani wa Dodoma.

Akizungumza na muakilishi news leo ofisini kwake amesema manispaa ya Dodoma imefanya maandalizi ya awali ikiwemo kupanda mitina kutoa elimu kwa jamii juu ya athari za ukataji wa miti nchini.

Aidha katika hatua nyingine amewataka viongoziwa ngazi zote kutoa elimu kwa wananchi ili kujuafaida ya upandaji wa miti.

‘’Unapomhamasisha mwananchi na akaelewa umuhimu itakuwa rahisikupanda misitu lakini kama hujui maana ya misitu ni nini, ataona kama unamtesa,’’alisema.

Pia ametoa ushauri kwa wananchi kutumia elimu watakayopewa na viongozi wao na kupanda miti kwa wingi ili kupata mvua kwa wakati kama Mikoa mingine.

Mbali na hayo Kabado amesema mkikakati iliyopo katika kupiga ukataji wa misitu ni pamoja na kuhakikisha kila kaya inapanda mitizaidi ya mitano , kuthibiti ukataji wa misitu na uchomaji wa mkaa ili kuweka utengamano wa mazingira .

‘’Kwanza tunaanza kwa kila kaya angalau ipande miti isiyopunguamitanokwa maana ya kwamba miti ya matunda miwili mitatu na miti ya kivuli miwili,’’ameongeza kusema Kabado.

Hata hivyo amewapongeza wananchiwanaondelea kutunza mazingira ikiwemo vyanzo vya maji ili kujiepusha na ukame kwaniMkoa wa Dodoma kwa sasa ni mkoa wenye watu wengi kutokana na kuwa makao makuu hivyo watu wengi kuongezeka.