- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ACT YAISHUTUMU SEREKALI KUPORA FEDHA ZA WAKULIMA WA KOROSHO
Dar es salaam: Chama cha ACT Wazalendo kimeishtumu serekali ya awamu ya tano kwa kushindwa kutoa fedha za wakulima za mazao ghafi ya Korosho yanayouzwa njee ya nchi yaani Export Levy kwa muda wa kipindi cha miaka miwili mfululizo yaani 2016/2017 na 2017/2018.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa Leo May 27, 2018 na Katibu wa Itikadi na Uwenezi wa ACT Wazalendo Ndg. Ado Shaibu inasema kuwa Sheria ya Korosho Na.18 ya mwaka 2009 ya Kifungu cha 17(A), kinaitaka serekali kutoa asilimia 65% ya tozo ya Export Levy kuingizwa kwenye Mfuko wa Bodi ya Korosho kwa ajili ya kugharamia uendeshaji wa zao hilo.
"Kwa mujibu wa taarifa ya Bodi ya Korosho, iliyotolewa kwa Kamati ya Bunge ya Maji, Kilimo na Mifugo, kwa msimu wa mauzo ya korosho wa 2016/2017 na 2017/2018, Bodi ilikuwa haijapokea jumla ya shilingi 211 bilioni (shilingi 91 bilioni kwa msimu wa 2016/2017 na shilingi 110 bilioni kwa msimu wa 2017/2018) kama makato ya 65% ya Export Levy kwa mujibu wa Sheria" ilisema sehemu ya Taarifa hiyo.
ACT imeyataja madhara ya kuchelewesha kutoa fedha hizo kwenye sekata ya korosho ambapo ni pamoja na Kupanda maradufu kwa bei ya pembejeo. "Bei ya pembejeo muhimu ya Salfa (Sulphur) kwenye maeneo mengi imepanda kutoka 16000 hadi 70000. Hii yote ni kwa sababu ununuaji wa pembejeo nje ya nchi unategemea kwa asilia 100 kutokana na Export Levy. Jambo hili lilitokea pia mwaka jana. Hivyo, gharama za uzalishaji kwa mkulima ni kubwa mno" amesema Ado
Aidha Kituo cha Utafiti Naliendele ambacho kinategemea fedha ya Export Levy kwa 90% katika kujiendesha kitashindwa kufanya kazi. Kituo hiki kinafanya kazi kubwa sana ya kufanya tafiti za mbegu bora za Korosho na dawa za kudhibiti magonjwa mbalimbali ya zao la korosho.
Pia sababu nyingine ni Bodi ya Korosho, ambayo ndiyo msimamizi mkuu wa zao la korosho nchini inashindwa kujiendesha kwa ufanisi, kwa sababu inategemea fedha hizi za export levy kwa 100% kujiendesha.
Mafunzo ya kilimo bora cha korosho kwa wakulima na maafisa ugani ambayo yanategemea Export Levy kwa 100% yamesimama kwa sasa.
Mwisho Kuvurugwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani kwa sababu usimamizi wa mfuko huo hutegemea fedha za Export Levy kwa 100%.
Imeandikwa na Issa Deyssa na kuhaririwa na Saada kimei
Muakilishi Publisher