Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 4:44 pm

NEWS: ''ACT WAZALENDO SIO CHAMA CHA KUISIFIA SEREKALI" ZITTO KABWE

Dar es Salaam: Mbunge wa Kigoama Ujiji na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe amesema chama chake siyo jukwaa sahihi la kuisifia Serikali kama wanachama wengine wanavyodhani.

Zitto ameyasema haya leo Juma tano (21.10.2017) wakati Akizungumza na waandishi wa habarii, kama kuna wanachama wanaodhani chama hicho ni jukwaa la kuisifia Serikali wajitathimini au kuchukua hatua kama wenzao walivyofanya.


Mkutano huu na waandishi wa habari umekuja siku chache tangu aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho, Samson Mwigamba na wenzake 10 kuhamia CCM
“Tulimwita Mwigamba katika kikao cha chama aje kutueleza kama tunakiuka misingi ya chama lakini hakufika. Chama kinaheshimu mchango wa kila Mwana-ACT, lakini tunawashauri wanaondoka wasiwashawishi wanachama wengine kuondoka,”
“Chama kimejiridhisha kwamba bado tunaendelea kusimamia misingi ikiwamo uzalendo sanjari na kupigania haki za demokrasia,”amesema Zitto

Zitto Amesema kuwa wanafanya yote hayo wakiongozwa na utu na uadilifu kama chama chao kinavyowaongoza.
“Chama chetu kina ahadi tano ambazo ni kupambana na rushwa na ufisadi na kamati ya uongozi imebaini kama haijatoka katika misingi yake kama wengine wanaoondoka wanavyodai,”amesema Zitto.


Amesema bado wanaendelea kupambana na umasikini na hali ya maisha kwa Watanzania wote.
“Hatujawahi hata siku moja kwenda kinyume na misingi ya chama hiki kama watu wanavyodai.”