Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 1:38 am

NEWS: ABURUZWA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA BINTI WA MIAKA 16

Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Said Mussa mkazi wa Makumbosho jijini Dar es salaam, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka 16 mkazi wa eneo hilo.

kwa mujibu wa Mwendesha Mashtaka, Credo Rugaju alidai mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Anifa Mwingira kuwa katika tarehe isiyofahamika mwaka huu eneo la Makumbusho, alimbaka binti wa miaka 16 (Jina limehifadhiwa).

Mshtakiwa alikana mashitaka na alishindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo alirudushwa rumande hadi Septemba 4 mwaka huu kesi itakapotajwa tena.

Wakati huohuo, mkazi wa Sinza Mori, Mohamed Hamis (24) amepandishwa kizimbani kwa shtaka la kukutwa na dawa za kulevya.

Mwendesha Mashtaka wa mahakama hiyo, Aboud Yusuph alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Boniphace Lihamwike, kuwa Januari 10, mwaka huu mshtakiwa alikutwa na Heroin Hydrochloride yenye uzito wa gramu 0.57.

Mshtakiwa alikana mashitaka na alirudishwa rumande hadi Septemba 3, mwaka huu kesi itakapotajwa tena.